Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mh Danstan Kyobya,katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya mji Nanyamba, amekutana na wenyeviti wa vijiji vyote vya halmashauiri ya Mji Nanyamba kwaajili ya kusikiliza kero. Wenyeviti wamesema kero kubwa kwao ni kukosa posho,kukosa bima za afya, vitambulisho walivyonavyo havina ubora na kuhitaji viboreshwe na wanahitaji mafunzo ya utawala bora.Halmashauri ya Mji Nanyamba ina jumla ya vijiji 87 na mitaa 9 na jumla ya kata 17.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amemwagiza mkurugenzi wa halmasahuri ya mji wa Nanyamba na manejimenti kuyafanyia kazi kero zote zilizotolewa na wenyeviti na kuzijibu kwa wakati.Pia ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi na wakuu wa idara kwenda vijijini kusikiliza kero na kutatua kero zote za kiutendaji.
mkuu wa wilaya amewaagiza wenyeviti wa vijiji kutekeleza jukumu la ulinzi na usalama katika maeneo yao na kutoa taarifa pindi wanapoona kunauhitaji wa kufanya hivyo.pili amewaagiza wenyeviti kusimamia miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika vijiji vyao kama vile zahanati,madarasa,ofisi za watendaji nk
mwisho mkuu wa wilaya amemwagiza mkurugenzi wa halmashauri ya mji Nanyamba kuuandaa ratiba na kumjulisha ili aweze kufanya ziara kwenye vijiji vyote kusikiliza na kutatua kero za wananchi,sambamba na kukaguamiradi yote ya maendeleo. ya halmashauri ya mji nanayamba yenye vijiji 87 na mitaa 9.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.