Ikiwa ni Miaka saba Mfululizo Bank ya @nmbtanzania Tawi la Nanyamba leo tarehe 14/11/2024 imeendelea na utoaji wa vifaa kutokana na faida inayopatikana kwa wateja wao ya asilimia 1 kwa mwaka wamegawa vifaa mbalimbali sekta ya Elimu na Afya katika Halmashauri ya Mji Nanyamba.Akisoma taarifa hiyo ya kukabidhi vifaa hivyo Meneja wa Nmb Kanda ya Kusini Bi Olipa Hebel jumla ya milioni 34.8 imetolewa kwa kununua vifaa kama vile Vitanda vya kujifungulia wajawazito, Magodoro, Madawati kwa shule za msingi, vitanda vya kawaida vya wagonjwa, viti na meza kwa shule za Secondari.Meneja wa Tawi la Nmb Nanyamba Ndg Mwabuke Mwakyusa amesema kuwa shule na sekta walionufaika na mgao huo kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ni Hospital ya Halmashauri Mji Nanyamba imepata vitanda 10 vya kawaida, Magodoro 10, vitanda 2 vya kujifungilia wajawazito, Kituo cha afya Dinyecha Magodoro 20, Kituo cha afya Nyundo Magodoro 6, Shule ya Msingi Mbembaleo madawati 50, Shule ya Msingi Njengwa madawati 50, shule ya Sekondari Mtiniko viti na meza 50, Shule ya sekondari Mnongodi viti na meza 50 na shule ya Sekondari Nyundo viti na meza 50.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba Mhandisi Mshamu Munde amewashukuru @nmbtanzania kwa kuendelea kurudisha faida kwa jamii ya Nanyamba hiyo imetokana na ushirikiano uliopo kati ya Nmb na jamii ya Nanyamba alimalizia kwa kusema hivyo.Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Nanyamba Mhe Jamali Abdalla Kapende kwaniaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara amewapongeza Nmb kwa kuendelea kutoa vifaa kwenye shule mbalimbali kupitia gawio hilo la faida aliwaeleza wasiwachoke Halmashauri wanavyoleta maombi yao ya kuomba msaada wa vifaa mbalimbali kupitia sekta hizo za afya na elimu kwani jambo wanalofanya ni kubwa sana kwa jamii ya wana Nanyamba kwa ujumla.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.