Chanjo ya Kuku Newcastle (Tatu moja) Kinga ya Kideri, Ndui na Mafua ya kuku imezunduliwa rasmi mapema hivi leo na Mkurugenzi wa Mji Nanyamba Bi Zainab Mgomi na itatolewa kwa siku saba kuanzia leo tarehe 14/7/2025 mpaka tarehe 21/7/2025 na Maafisa Mifugo wakishirikiana na Viongozi wa Kata,Vijiji,Mitaa na Vitongoji mpaka itakapo kamilika .
Katika ufunguzi wa zoezi hilo Bi Zainabu ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania @samia_suluhu_hassan kwa kugharamia chanjo hizi kwa wananchi wote ambazo zitatolewa kwa Miaka Mitano mfululizo bila ya malipo na amewataka Maafisa Mifugo hao Kuchanja Kuku zote ambazo hazina ugonjwa na kukusisitiza kuwa chanjo ni kinga kwa kuku zote ambazo hazina maambukizi.
Matarajio ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba kuwa zoezi hili litafanikiwa kwa waledi kwa kufuata muongozo wa Serikali kama ulivyotolewa hivyo Wananc hi wote mnaombwa kutoa ushirikiano wa dhati kuhakikisha chanjo inamfika kila mfugaji kwa mujibu wa ratiba ya chanjo ikiwapo na kufuata maelekezo na mafunzo yote kwa wataalamu wa mifugo
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.