MKurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba Bi Zainab Mgomi, Leo tarehe 22 julai 2025 ametambulisha rasmi miradi ya maendeleo ya mpango wa BOOST kwa miradi ya ujenzi wa shule ya awali ya mkondo mmoja shule ya msingi Namtumbuka kutokana na shule iliyopo ni ya muda mrefu hivyo miundombinu yake ni chakavu, pia ujenzi wa shule ya msingi na awali ya mkondo mmoja ndani ya shule ya sekondari Nitekela.
Akizungumza wakati wa utambulisho wa miradi, mkurugenzi wa Mji amemshukuru Mh Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa Nanyamba kwa kuleta pesa kiasi Cha Tsh bilioni 1.32 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo sekta ya Elimu ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia,
vijiji vya Namtumbuka na Nitekela kila kimoja kitaenda kutekelezwa miradi ya Tsh milioni 314 ili kukamilisha ujenzi wa miradi tajwa.
Aidha ametoa wito kwa wote watakaohusika kwenye zoezi la utekelezaji miradi kwa upande wa wataalam ngazi ya Halmashauri na timu za ufuatiliaji na upokeaji vifaa kwa ngazi ya vijiji kuwa wazalendo na waadilifu ili kukamilisha miradi kwa wakati na ubora inayoendana na thamani ya pesa iliyotolewa na serikali.
Mratibu wa mpango wa BOOST ndugu Mohamedi Kazumari aliwaomba wananchi kushiriki katika hatua za awali kama vile usafishaji wa eneo la mradi na uchimbaji wa msingi ikiwa ni sehemu ya mchango wa jamii katika miradi ya maendeleo.
Akizungumza katika zoezi la utambulisho wa mradi afisa elimu msingi ndugu Joseph Muhagama aliwaasa walimu viongozi na timu za Usimamizi ngazi za vijiji kuhakikisha mchakato wa manunuzi unatumia mfumo wa NeST kama miongozo ya serikali inavyoelekeza lakini pia waweke rekodi ya taarifa na nyaraka zote za miradi kwa usahihi .
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.