Mapema hivi leo Watumishi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba na taasisi mbalimbali za serikali walijumuika kwa furaha kwenye bonanza la michezo lililolenga kuimarisha mshikamano, ushirikiano kazini na afya za wafanyakazi.Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Abdallah Mwaipaya, akiongozana na Katibu Tawala wa Wilaya Wakili Richard Mwalingo pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba Bi Zainab Mgomi.Bonanza hilo lilianza na Jogging mapema asubuhi ya leo bila kusahau Michezo mbalimbali ilifanyika ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete, kuvuta kamba, mpira wa wavu, mbio na zawadi mbalimbali zikitolewa kwa washindi. Ushindani wa kirafiki ulitawala huku washiriki wakionyesha umoja na mshikamano wa kipekee.Akihutubia, Mhe. Mwaipaya aliwapongeza watumishi kwa mshikamano na ushiriki wao, akisisitiza kuwa michezo ni njia bora ya kujenga afya, kuongeza ari ya kazi na kudumisha mshikamano wa kitaifa pia alisisitiza kuwa mashindano haya yawe endelevu ili kuimarisha zaidi mahusiano kazini.Bila kusahau katibu tawala waWilaya na Mkurugenzi waliweza kutoa neno kwa kuwashukuru Watu wate waliojitokeza kwa siku ya leo katika zoezi hili muhimu la kujenga afya na kuimarisha urafiki na ushirikiano
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.