Zikiwa zimesalia siku chache kuazimisha siku ya Wanawake Duniani tarehe 14/2/2024 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba kumefanyika kikao cha jukwaa maalumu la Wanawake katika kujadili maendeleo, uhai na changamoto zinazokumbana na majukwaa yote ya Halmashauri ya Mji Nanyamba.
Aidha jukwaa hilo la Wanawake mambo Mengi yalijadiliwa kwa lengo la kuendeleza maendeleo ya Wanawake Halmashauri ya Mji Nanyamba ikiwa pamoja na malengo yao muhimu kwa kila kiongozi wa kila kata katika kuchangia ukuaji wa majukwaa ya Wanawake Halmashauri ya Mji Nanyamba ikiwa pamoja na
-Viongozi wa kata kufanya ziara za kutembela majukwaa yote ndani ya kata
-Kutafuta rasilimali fedha, watu na vitendea kazi vitakavyo saidia katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali.
- Kuanzisha miradi ya maendeleo ya kimkakati ili kuongeza kipato cha jukwaa.
- Kusimamia uhai na maendeleo ya jukwaa kuanzia ngazi ya mtaa na kijiji.
- Kuanzisha vikundi mbalimbali vya maendeleo katika maeneo ambako hakuna vikundi
Jukwaa hilo limesimamiwa na Bi Shadia Amour ambaye ni Mwenyekiti wa jukwaa ngazi ya Halmashauri.
Jukwaa hilo la Wanawake lilihudhuliwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Asha mfaume katibu wa jukwaa Halmashauri ya Mji Nanyamb , Fatuma fujo Makamu Mwenyeikiti ngazi ya Halmashuri, wawakilishi kutoka Benki za CRDB na NMB , pamoja na Viongozi mbalimbali wa majukwaa ya kata ya Halmashauri.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.