Kituo cha afya Dinyecha kilichopo Halmashauri ya Mji Nanyamba, kilianza kutoa huduma Septemba 2013 kama “Zahanati ya kijiji” kabla ya kupandishwa hadhi mwaka 2017 na kuwa “Kituo cha Afya” ambapo leo tarehe 15 Septemba 2023 kimeadhimisha miaka 10 tangu kuanza kutoa huduma ya afya.
Dkt. Jeremiah Sebastian, mganga mfawidhi wa kituo hiko ameelezea mafanikio ya kituo ambapo amesema tangu kuanza kutolewa kwa huduma za upasuaji mwaka 2019 wameweza kuhudumia wagonjwa 1171; ambapo kati ya hao 1010 ni mama wajawazito huku 161 ni upasuaji wa magonjwa mengine.
Dkt. Jeriamiah aliendelea kueleza mafanikio ya kituo hiko cha afya ambapo alibainisha kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kituo kimeweza kukusanya mapato ya ndani zaidi ya shilingi milioni 138.
Akizungumzia hali ya upatikani huduma, mganga huyo mfawidhi alisema kituo kinatoa huduma OPD , upimaji wa maabara, kulaza na upasuaji. Aidha aliongeza kuwa kwa sasa kituo kina watoa huduma 46, ambapo kati ya hao 30 ni wa kuajiriwa na 16 ni wa kujitolea.
Kauli mbiu ya Kituo cha afya Dinyecha ni “Afya yako kipaumbele chetu”.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.