Miradi sita ya maendeleo inayotekelezwa katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2023/24 ndani ya Halmashauri ya Mji Nanyamba leo tarehe 26/01/2024 imetembelewa na kamati ya Fedha, Utawala na Mipango.Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Nanyamba, Mhe. Jamal Kapende wametembelea na kukagua Ujenzi wa Zahanati ya Kiromba chini, Ukamilishaji wa Madarasa matatu ya shule ya sekondari Kiyanga, barabara za jamii kijiji cha Magomeni, Ujenzi wa shule mpya ya sekondari Hinju.
Aidha, kamati imetembelea na kukagua kikundi cha Pambamoto kinachoendesha biashara ya vifaa vya ujenzi pamoja na kiwandani cha uchakataji na ukamuaji wa mafuta ya alizeti baada kupatiwa mkopo wa Milioni 50.17 kutoka Halmashauri. Pia kamati hiyo imetembelea na kukagua shule ya mchepuo wa kingereza (English medium) Namkuku.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.