Halmashauri ya Mji Nanyamba ilianzishwa rasmi mwezi Julai, 2015 kwa Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) namba 8 ya mwaka 1982 kwa Tangazo la Serikali Namba 220 la tarehe 05/06/2015. Madhumuni halisi ya kuanzishwa Kwa Halmashauri ya Mji Nanyamba ni kusogeza karibu na wananchi huduma mbalimbali za kiuchumi na kijamii zikiwemo sekta za Maji, kilimo, Elimu, Barabara, Afya pamoja na kuboresha miundombinu iliyopo kwa manufaa ya wananchi wa Nanyamba.
Halmashauri ya Mji Nanyamba ni miongoni mwa Halmashauri tatu zilizo katika Wilaya ya Mtwara. Kwa upande wa Kaskazini Mashariki inapakana na Halmashauri ya Wilaya Mtwara. Magharibi inapakana na Wilaya ya Tandahimba na Mkoa wa Lindi. Kusini Nchi ya Msumbiji. Makao Makuu ya Halmashauri yapo katika kata ya Nanyamba, Jimbo la uchaguzi lipo moja la Nanyamba ,Tarafa 3 kata 17 vijiji 87 mitaa 9 na vitongoji 323.
MAHAKAMA
Halmashauri ya Mji Nanyamba inatumia Mahakama ya Wilaya ya Mtwara pamoja na Mahakama za Mwanzo mbili ambazo ni Nanyamba na Kitaya
HALI YA UPATIKANAJI WA CHAKULA.
Kwa kipindi hiki Wananchi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba wanaendelea na shughuli ya kilimo cha mazao ya muda mfupi kama njugu mawe, karanga, mpunga, mbaazi, mahindi, mtama, kunde, ufuta pamoja na maandalizi ya mashamba ya mikorosho hasa kwa kazi za upuluziaji wa dawa za magugu.
Aidha vyakula vya aina mbalimbali vinapatikana majumbani, kweye masoko na magengeni. Vyakula vya aina ya wanga vinavyopatikana ni pamoja na Mchele, Makopa (mihogo), Mahindi (sembe) na Mtama. Pia mboga za majani za aina mbalimbali zinapatikana zikiwemo bilinganya, bamia, matembele, mchicha, kisamvu (majani ya muhogo), chainizi na nyanya maji. Baadhi ya Matunda kama nanasi na mastafeli yanapatikana.
HALI YA MIUNDOMBINU YA BARABARA
Halmashauri ya Mji wa Nanyamba ina barabara zenye urefu wa km 498.85 kuna barabara za Mkoa zenye urefu wa Km. 82.8 na Barabara za Halmashauri ya Mji Nanyamba zenye urefu wa Km 416.05 hivyo kufanya Halmashauri ya Mji wa Nanyamba kuwa na barabara zenye urefu wa km 498.85 Mtandao Huu wa barabara ambao hupitika kipindi chote cha Mwaka. Mtandao huu wa barabara huwasaidia wananchi kusafiri na kusafirisha bidhaa zao kwa vyombo vya usafiri wa magari ya mizigo, mabasi, baiskeli na Pikipiki.
HALI YA MASOKO NA HADHI ZAKE.
Shughuli za biashara (masoko) zinazopatikana au zinazoendelea ni pamoja na biashara za mazao mchanganyiko, Maduka rejereja, hivyo uwepo wa shughuli hizo umesababisha Halmashauri kupata mapato kupitia tozo mbalimbali kama kodi ya ushuru wa bidhaa, ushuru wa masoko na leseni za biashara.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.