Wananchi kwa kushirikiana na watumishi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba wameadhimisha Siku ya Usafishaji Duniani kwa kufanya usafi katika Kituo cha Afya Dinyecha. Zoezi hilo limekusudia kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kulinda mazingira ili kuhakikisha afya bora na maisha yenye ustawi.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, viongozi wa Halmashauri wamesisitiza kuwa jukumu la kulinda mazingira ni la kila mmoja, na ushirikiano kati ya wananchi na watumishi unaleta matokeo chanya kwa maendeleo ya jamii. Aidha, wananchi waliojitokeza wamesema wanatambua umuhimu wa kushiriki katika shughuli hizo, kwani mazingira safi ni msingi wa afya bora na kupunguza magonjwa ya mlipuko.
Maadhimisho ya Siku ya Usafi Duniani hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuelimisha na kuhamasisha jamii duniani kote kuhusu wajibu wa kulinda mazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.