Kitengo cha ukaguzi wa ndani kimeanzishwa chini ya kifungu 45 (1) cha sheria ya fedha ya mamlaka ya Serikali za mitaa Na 13 ya mwaka 1982.Kitengo hiki kinatekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na Kamati ya Ukaguzi.
Kazi za Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani.
Kukagua na kutoa ushauri sahihi ili kuboresha utawala bora.
Kufanya ufuatiliaji , ukaguzi na usimamizi wa fedha zote za Halmashauri ili kuangalia kama zinakusanywa na halmashauri kwa kutumia mifumo ya kieletroniki.
Kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha zote za Halmashauri na kuandaa taarifa na kuikabidhi kwa Afisa Masuuli.
Kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na mali za Halmashauri pamoja na kuhakiki uwepo wa thamani ya fedha.
Kuhakikisha kama malengo ya halmashauri yanafikiwa na kuangalia kama upo uwajibikaji katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya Halmashauri.
Kuhakikisha kuwa sheria, kanuni na taratibu za fedha za serikali zinafuatwa kama zilivyo ainishwa kwenye sheria mbalimbali za serikali.
Kupitia na kutoa taarifa juu ya majibu ya menejimenti kwenye taarifa za ukaguzi wa ndani na kuisaidia menejimenti kwenye utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa kwenye taarifa mbalimbali na ufutiliaji kwenye utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.