Leo katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Nanyamba kimefanyika kikao cha wadau wa zao la korosho kwa lengo la kujadili ufanisi na tija ya msimu wa kilimo mwaka 2025/2026.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Nanyamba, Bi. Zainab Mgomi, alimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mheshimiwa Abdallah Mwaipaya, ambaye aliongoza kikao hicho kama mwenyekiti.Katika kikao hicho, maafisa mbalimbali wa Halmshauri na sekta ya kilimo walifanya mapitio na mawasilisho kuhusu ubora wa zao la korosho, hatua zilizochukuliwa kuongeza ufanisi, na mikakati ya kuimarisha thamani ya zao hilo.Pia Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha Korosho Halmshauri ya Mji Nanyamba aliwasilisha taarifa kuhusu hatua za uthibiti wa zao hilo, huku wananchi wakipata nafasi ya kutoa mawazo yao juu ya namna ya kuboresha sekta hiyo muhimu kwa uchumi wa taifa ndani ya halmshauriViongozi wengine waliotoa nasaha na ushauri mbalimbali ni pamoja na Katibu Tawala wa Wilayaya Mtwara, Wakili Richard Mwalingo, Mrajis wa Mkoa wa Mtwara, Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Mtwar-Masasi Mamcu ,Meneja wa Uthibiti Ubora wa Korosho wa Mtwara, pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali za kifedha ikiwemo NMB, CRDB na DCB Bank Pia walihudhuria viongozi wengine wa kada mbalimbali.Dc Mwaipaya alihitimisha kikao kwa kutoa hotuba fupi akiwataka viongozi wote kuhakikisha wanachukua hatua madhubuti katika kusimamia zao la korosho ili kuongeza tija na kipato cha wakulima wa Nanyamba na taifa kwa ujumla.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.