74 WAPATA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI NANYAMBA
Wahasibu na Makatibu 74 kutoka Vikundi 37 vya Wajasiriamali Halmashauri ya Mji Nanyamba wamepata mafunzo ya Ujasiriamali kutoka kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mji Nanyamba.
Ofisi ya Mkurugenzi wa Mji Nanyamba chini ya Idara ya Maendeleo ya Jamii, wameendesha mafunzo ya Ujasiriamali kwa vikundi vya wajisiamali huku mafunzo hayo yakihusisha makatibu na wahasibu. Katika mafunzo hayo yaliyofanyika tarehe Machi 14, 2018 katika Shule ya Sekondari ya Kutwa Nanyamba.
Katika mafunzo hayo, ambayo yalifunguliwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii Mheshimiwa Jafari Hasani Mwihumbo (Diwani), wawezeshaji waliwasilisha mada tatu; 1. Ujasiriamali ambapo makatibu na wahasibu walielezwa namna ya kuibua miradi, 2. Mapato na Matumizi ambapo wahasibu walielezwa matumizi yasizidi kipato na 3. Sheria ambapo mafunzo yalijikita katika namna ya kujaza mikataba na kanuni za urejeshaji wa fedha.
Aidha, wawezeshaji waliwataka wahasibu na makatibu kujikita Zaidi katika kuibua miradi mbalimbali kama sehemu ya kuvipa uhai vikundi hivyo.
Tayari hadi sasa, Halmashauri ya Mji Nanyamba imeshatoa mikopo ya fedha kiasi cha Shilingi 114,540,000/= kwa vikundi vya Ujasiriamali 37 kutoka kwenye chanzo cha mapato ya ndani.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.