Baraza la Waheshimiwa Madiwani Halmashauri ya Mji Nanyamba leo tarehe 30/1/2025 limepitisha Mpango wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 24.4.Akisoma taarifa hiyo Mkurugenzi wa Mji Nanyamba Mhandisi Mshamu Munde amesema kuwa makisio ya mpango wa bajeti ni shilingi bilioni 24.4 ambapo Ruzuku ya mishahara ni shilingi bilioni 13.3 sawa na asilimia 55.1, Ruzuku ya miradi ya maendeleo shilingi bilioni 1.024 sawa na asilimia 4.2, mapato ya ndani shilingi bilioni 3.7 sawa na asilimia 15.2 na michango ya jamii katika shughuli za maendeleo shilingi milioni 250 sawa na asilimia 1.0.Aidha Mkurugenzi baada ya kuwasilisha mpango huo wa bajeti alisema bajeti hii imekuwa na ongezo la shilingi bilioni 1.2 sawa na asilimia 5.6 ukilinganisha na bajeti ya mapato ya mwaka 2024/2025 yenye jumla ya makadirio ya shilingi bilioni 23.1.Mpango huo wa bajeti umepitishwa katika Mkutano maalum wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba kuhudhuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Abdallah Mwaipaya, kamati ya Usalama, viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa wakuu wa Taasisi za Serikali, Maafisa Tarafa, wakuu wa Divisheni na vitengo pamoja wa watendaji wa kata.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.