Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba, Bi. Zainabu Mgomi, ameshiriki zoezi la uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Namtumbuka.
Ushiriki wake unalenga kuhamasisha wananchi kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo hususan ya elimu, ambayo ni chachu ya kuinua kiwango cha taaluma kwa watoto wa Nanyamba.
Katika hotuba yake, Bi. Mgomi amewaomba wananchi kuendelea kushirikiana katika miradi yote ya maendeleo, akisisitiza kuwa mshikamano wa jamii na Serikali ni nguzo muhimu ya kufanikisha malengo ya kuinua huduma za kijamii na kuboresha maisha ya wananchi.
Aidha, wananchi wamempongeza kwa uongozi wake shirikishi na ari ya kuhakikisha kila mtoto anapata fursa ya kusoma katika mazingira bora, wakiahidi kuendeleza mshikamano na mshirikiano katika miradi yote ya kijamii.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.