Mnamo tarehe 11 Julai 2025 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba @mgomizainab amekabidhiwa ofisi na mtangulizi wake Mhandisi @mshamu__munde
Aliyemaliza muda wake wa Kiutumishi mbele ya Timu ya Menejimenti katika ukumbi mdogo wa Halmashauri.
Mhandisi Mshamu Munde akikabidhi ofisi hiyo amewashukuru Timu ya Menejimenti kwa ushirikiano kipindi chote cha majukumu yake ya Ukurugenzi wamempa ushirikiano wa kutosha na waendelee na kasi hiyo hiyo ya ushirikiano.
Aliendelea kwa kusema kuwa yeye anaoandoka hatarajii kusikia kuwa Mkurugenzi aliyeondoka alikuwa hivi wachuku yale mazuri na mabaya wamuachie yeye mwenyewe ili Halmashauri ya Mji Nanyamba iendelee kusonga kimaendeleo.Kwa upande wa Mkurugenzi Bi Zainab S. Mgomi alimshukuru mtangulizi wake kwa mapokezi mazuri toka anakuja kuripoti na ifmefikz hatua ya makabidhiano unajua mchango wake kiutumishi ataendelea kuchota busara, ushauri ili Nanyamba iweze kukuwa kiuchumi na katika nyanja mbalimbali.
Pia alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt @samia_suluhu_hassan kwa kumuamini na kumpa majukumu hayo ili aweze kuisimamia vyema Halmashauri ya Mji Nanyamba ipasavyo.
Timu ya Menejimenti imemtakia safari njema Mhandisi Munde nje ya Utumishi wake uliofikia kikomo na kumkaribisha Mkurugenzi Bi Zainab kwa kusema kuwa wapo Tayari muda wote kufanya kazi iwe jua, iwe mvua ili kuendelea kusongesha gurudumu la kimaendeleo
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.