Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba, Bi Zainabu Mgomi, amekabidhiwa jezi leo ofisini kwake na Afisa Michezo Yahaya Athumani Kibaraka, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kushiriki katika jogging.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa jezi hizo, Bi Zainabu Mgomi amewataka wananchi wa Nanyamba kujitokeza kwa wingi kushiriki michezo, akibainisha kuwa michezo ni nyenzo muhimu ya kuimarisha afya, mshikamano na mshikamo wa kijamii.
Aidha, ameahidi kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo na kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha michezo inakuwa endelevu na yenye manufaa kwa jamii.
Jogging hiyo inatarajiwa kuwakutanisha wananchi kutoka makundi mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, watumishi wa umma na wadau wa michezo, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utamaduni wa kufanya mazoezi na kuimarisha afya.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.