CMT YATEMBELEA KITUO CHA AFYA DINYECHA
Timu ya wataalam ya Halmashauri ya Mji Nanyamba ambayo inaumdwa na Wakuu wa Idara ikiongozwa na Mkurugenzi wa Mji Ndg. Oscar A. Ng’itu, Septemba 28 ilitembelea na kukagua kituo kipya cha afya cha Dinyecha ili kujionea shughuli mbalimbali zinazoendelea Kituoni hapo pamoja na huduma kutolewa kituoni hapo.
Mkurugenzi wa Mji Wakili Msomi Oscar A. Ng'itu (Aliyevaa suruali yenye rangi ya damu za mzee) akiongozana na Mganga Mkuu wa Mji Dkt. Kyabaroti P. Kyabaroti.
Timu hiyo ambayo iliongozwa na Mkurugenzi wa Mji ilianza kukagua Duka la dawa la Halamashauri lililopo kituoni hapo ambapo mambo mbalimbali yaliweza kuelezwa kama ushauri katika usimamaizi na uendeshaji wa duka hilo.
Muonekano wa nje wa dula la dawa linalomilikiwa na Halmashauri ya Mji Nanyamba
Aidha, mfamasia wa Mji Ndg. Emanuel Maro aliieleza CMT mipango mikakati wa namna ya uendeshaji wa duka hilo huku akieleza manufaa ambayo Halmashauri na Jamii itafaidika kupitia duka hilo. Uwepo wa duka hilo utapunguza kero ya wananchi kusafiri kwenda Mtwara mjini kununua dawa badala yake dawa zitapatikana hapa hapa.
Mfamasia wa Mji Ndg. Emanuel Maro (mwenye shati jeupe) akiwa anaeleza namna gani duka hilo linafanya kazi
Pia, CMT ilitembelea chumba cha kuhifadhia dawa, vyumba vya kutolea huduma kama vile vyumba vya waganga na kile cha sindano ili kuweza kujionea utaratibu uliopo ambapo Mkurugenzi wa Mji aliwashauri wahusika kuweka utaratibu mzuri wa mpangilio wa uhifadhi wa maboksi ya dawa na vifaa vinginevyo.
Mkurugenzi wa Mji akipokea maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu
Katika kuhitimisha ziara hiyo, timu hiyo ilimshauri mganga mfawidhi kuhakikisha wanaweka utaratibu mzuri wa utoaji huduma ambapo wagonjwa watapata huduma bora kwa wakati bila kusumbuka.
Kwa picha za matukio mbalimbali bofya http://nanyambatc.go.tz/sinlge-gallery/cmt-yatembelea-kituo-cha-afya-dinyecha
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.