Benki ya Crdb tawi la Nanyamba leo tarehe 6/10/2023 wamekabidhi meza 50 na Viti 50 kwa Shule ya Sekondari Mnyawi Kata ya Milangominne katika kuelekea kilele cha wiki ya huduma kwa wateja.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Afisa Mahusiano Biashara za Serikali Kanda ya kusini Ndg. Alpha Mhagama amesema kuwa lengo Kuu la kukabidhi meza na Viti ni kuunga juhudi za Serikali katika Uboreshaji wa miundombinu ya elimu kwa wanafunzi.
Kwa niaba ya Meneja wa Benki ya Crdb tawi la Nanyamba, Bi. Clara Mwakabonga ameishukuru Serikali na Menejimenti ya Halmashauri Mji Nanyamba kwa ushirikiano wao na kuahidi kusaidia zaidi katika sekta zingine pia ikiwemo vile Afya, Kilimo na Utawala.
Kwa upande wa wanafunzi wa Shule hiyo ya Mnyawi Sekondari Wameishukuru Benki ya Crdb Tawi la Nanyamba kwa kuwajali kuwaletea Viti na meza.
Aidha, Benki ya Crdb Tawi la Nanyamba wameshiriki pamoja na Menejimenti ya Halmashauri Mji Nanyamba pampoja wateja katika Chai ya asubuhi.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.