FAINI YA MILIONI 10 KWA WATAKAOFANYA MANUNUZI YA UMMA NJE YA MFUMO WA NeST.
Mamlaka ya udhibiti manunuzi ya umma (PPRA) imetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa umma 60 wa idara na vitengo mbalimbali kutoka Halmashauri ya Mji Nanyamba, Manispaa ya Mtwara Mikindani na Wilaya ya Mtwara kuhusu mfumo mpya wa manunuzi ya umma kieletroniki, NeST. Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Boma, ofisi ya mkuu wa mkoa Mtwara kuanzia tarehe 21/08/2023 na kumalizika tarehe 25/08/2023.
NeST (National e-procurement system Tanzania) ni mfumo mpya wa manunuzi ya umma kielotroniki ambao utanza kutumika kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ukichukua nafasi ya mfumo wa awali ujulikanao kama TANePS baada ya serikali kuona kwamba mfumo huo ulikuwa na mianya inayochelewesha huduma.
Waratibu wa mafunzo hayo waliwataka washriki wa mafunzo hayo kuzingtia kwa makini ili waweze kuufanyia kazi watakaporejea kwenye vituo vyao kwani hakutakuwa na manunuzi ya umma yatakayofanyika nje ya mfumo wa NeST.
Aidha, waratibu ho walisisitiza kuwa faini ya milioni 10 itatozwa kwa watakaofanya manunuzi ya umma nje ya mfumo wa NeST. Akizungumza kwa niaba ya Halmashauri ya Mji Nanyamba, afisa manunuzi Bw. Seif Mrisho alielezea faida za mfumo huo ikiwemo uwazi wa tenda kwa wazabuni na kueleza kuwa Halmashauri ya Mji Nanyamba iko tayari kuanza kutumia mfumo mpya wa NeST.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.