Halmashauri ya Mji Nanyamba katika kuadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama Duniani,Elimu imeendelea kutolewa kwenye vituo vya afya na kwenye jamii kwa wakinamama wajawazito na wale wanaonyonyesha, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha afya ya mama na mtoto. Maadhimisho haya ambayo huadhimishwa kila mwaka kuanzia Agosti 1 hadi 7 yanalenga kuhimiza jamii kuelewa na kuthamini mchango mkubwa wa unyonyeshaji katika maisha ya mtoto na familia kwa ujumla.Leo tarehe 5/8/2025 maafisa lishe Halmashauri ya Mji Nanyamba wametembelea kata ya Mnongodi, kijiji cha Mnongodi na Mnongodi magharibi kutoa elimu kuhusiana na unyonyeshaji. Ambapo, elimu kuhusiana na faida za kunyonyesha kwa mama na mtoto, mambo ya kuzingatia wakati wa kunyonyesha, dhana potofu kuhusiana na unyonyeshaji ilitolewa.Dhima ya Wiki ya Unyonyeshaji kwa mwaka huu inasema: “Thamini Unyonyeshaji: Weka Mazingira Wezeshi kwa Mama na Mtoto.” Kauli mbiu hii inalenga kuchochea juhudi za pamoja katika familia, jamii, na serikali kuhakikisha mama anapokea msaada wa kutosha ili aweze kunyonyesha bila vikwazo. Mazingira haya ni pamoja na upatikanaji wa taarifa sahihi, msaada wa kihisia, muda wa kutosha wa likizo ya uzazi, na huduma bora za kiafya.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.