Kupitia Divisheni ya Afya Mji Nanyamba inahakikisha wananchi wanahamasika kuchangia damu safi na salama, Halmashauri ya Mji Nanyamba imeibuka kidedea robo nne Mfululizo na kuzipiku Halmashauri zote zilizopo ndani ya Mkoa wa Mtwara kuwa vinara wa uchangiaji damu Kimkoa.
Akikabidhi kombe la Ushindi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Dkt Benedicto Ngaiza ameipongeza Halmashauri ya Nanyamba kwa kuonesha juhudi za kutoa hamsakwa wananchi juu ya umuhimu wa kuchangia damu, alisema kuwa wale wanaochangia damu wakipatwa na changaya damu wao au ndugu zao wapewe kipaumbele kwasababu damu hizo haijulikani nani zitamsaidia na wakati gani.
Aliendelea kwa kusema Halmashauri zingine za Mkoa huo ziige mfano wa uhamasishaji wanaotumia Nanyamba kwa wananchi wao, Zawadi hiyo ya kombe ilipokelewa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Nanyamba Dkt Dickson Masale pamoja na timu yake ya CHMT.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.