Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Nanyamba Ndugu,Geophrey Martini amewasilisha taarifa ya miradi mbalimbali ya maendeleo mbele ya Mhe. Naibu waziri (MB) Mwita Waitara wakati alipotembelea Halmashauri ya Mji Nanyamba tarehe 10/03/2019.
Awali akimkatribisha Naibu Waziri, Kaimu Mkurugenzi alimweleza mafanikio mbalimbali ambayo Halmashauri imeyapata tangu kuanzishwa kwake mwaka 2015, ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za Afya, Kilimo,Elimu,Mifugo matumizi mazuri ya Aridhi na mazingira, uwezeshaji vikundi na mambo mengine.
Pia hakusita kumweleza changamoto mbalimbali ambazo halmashauri inaendelea kuzifanyia kazi na kutafuta ufumbuzi kama vile upungufu wa watumishi na uboreshaji wa miundombinu ya utendaji kazi ili kuweza kuwafikia wananchi wote kwa wakati.