Ikiwa ni wajibu wa kamati ya Fedha, Utawala na Mipango kila robo ina wajibu wa kukagua na kutembelea miradi inayotekelezwa ndani ya Halmashauri ya Mji Nanyamba ikiwa leo tarehe 22/1/2025 imefanya ukaguzi wa miradi mbalimbali katika sekta ya afya na elimu.Ziara hiyo ya kamati ya fedha, Utawala na Mipango imetembelea miradi yenye thamani ya bilioni 1.3 katika sekta afya na elimu, miradi iliyotembelewa ni mradi wa Sekondari mpya kata ya Hinju kupitia mradi wa uboreshaji wa elimu Sekondari (SEQUIP), mradi wa kituo cha afya Nyundo, ujenzi wa shule mpya ya mkondo mmoja Shule ya Msingi Nyundo B, ukarabati wa shule ya Msingi Nitekela.Kamati ya fedha katika ziara hiyo imeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Nanyamba Mhe Kapende aliwahimiza timu ya Menejimenti wahakikishe miradi yote waliyotembelea ikamilike kwa wakati kama walivyotoa ahadi mbele ya kamati hiyo.Aidha kamati hiyo imefurahishwa na hali ya miradi inavyoendelea kutekelezwa kutokana na kukidhi ubora wa viwango vya ujenzi unavyotakiwa na serikali walielezwa mafundi hao kuendelea kusimamia ubora wao wa kazi wanazopatiwa kutekeleza.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.