Katika kufanikisha shule mpya ya Sekondari Hinju iliyopo kata ya Hinju inajengwa kwa ustadi na ubora wenye viwango unaotakiwa na Serikali leo tarehe 10/1/2025 kamati ya Siasa Mtwara Vijijini imetembelea na kuona hali ya ujenzi wa shule hiyo.
Akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa shule hiyo mpya Mkuu wa Shule ya Hinju Mwl Fidelia E. Kagombe alisema kuwa kupitia mradi wa matokeo ya Utekelezaji wa Mpango wa Uboreshaji wa Elimu ya Sekondari Nchini (SEQUIP awamu ya tatu) Halmashauri ya Mji Nanyamba ilipokea kiasi cha shilingi milioni mia tano sitini elfu laki tano hamsini mbili mia nane ishirini na saba (560,552,827).
Hadi kamati ya siasa inatembelea mradi huo kuona hali ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inatekelezwa ipasavyo ziara hiyo ikiongozwa na Katibu Mwenezi wa Mtwara Vijijini Ndg Hamisi M. Wanyama wameridhishwa na ubora wa mradi huo na thamani ya fedha inavyotumika inaendana na thamani yake.
Aidha aliendelea kwa kusema kuwa ubora huo na miradi mingine inayoendelea kujengwa iendelee kusimamiwa ipasavyo, mradi huo wa shule ya Hinju unatarajiwa kukamilika tarehe 31/1/2025 ili uanze kutumika, mradi huo miundombinu yake ni kama kichomea taka, tank la maji la Ardhini, matundu nane ya Vyoo, chumba cha Tehama, jengo la Maktaba, jengo la Maabara ya Fizikia, Biolojia na Kemia, jengo la utawala pamoja na vyumba vya madarasa manne.
Kamati ya siasa kata ya Hinju ikiongozwa na Diwani wa kata hiyo Mhe Ngongo ameishukuru Serikali chini ya Rais Dkt Mhe @samia_suluhu_hassan na Mbunge wa jimbo hilo mhe @chikota_abdallah kwa juhudi zao za kuwaletea maendeleo kwenye kata hiyo.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.