Katika kuhakikisha Halmashauri ya Mji Nanyamba unakuwa Mji wa kisasa leo tarehe 5/12/2024 kampuni ya @afrosolar_tz ya jijini Dar es Salaam imeingia mkataba na Halmashauri ya ufungaji wa Taa za Barabarani.
Ufungaji huo wa taa za barabarani jumla ya taa 132 zenye thamani ya milioni 459.2 zaidi ya kilomita 11 za Mji Nanyamba zitafungwa taa hizo, akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Ndg Ambrosi Shayo watahakikisha taa hizo zinafungwa kwa wakati ili Mji wa Nanyamba uweze kufanya shughuli zake za kiuchumi kwa masaa yite yaani usiku na mchana.
Mkurugenzi wa Mji Nanyamba Mhandisi Mshamu Munde amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Mhe Abdallah Dadi Chikota kwa juhudi zake za kuibadili Halmashauri ya Nanyamba kuwa ya kisasa na ya kipekee kwa mkoa wa Mtwara na hata mikoa mingine.
Mkurugenzi Munde alizitaja barabara zitakazopitiwa na mradi huo ni barabara ya Hawa Ghasia, barabara ya Chikota, barabara ya Kinondoni, barabara ya Msijute, barabara ya Kitaya pamoja na barabara ya Nitekela.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.