Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Ahmed Abbas amefungua kikao kazi cha mkoa Mtwara kujadili vifo vya akina mama na watoto wachanga vitokanavyo na uzazi, kilichoanza Leo tarehe 24/01/2024 Halmashauri ya Mji Nanyamba.Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hiko, Kanali Abbas amewataka wakurugenzi watendaji wa Halmashauri kugharamia mafunzo yanayoratibiwa na mkoa kwa kada mbalimbali yanayolenga kuboresha huduma za uzazi salama.
“Kifo cha mama kinachotokana na uzazi niwe napatiwa taarifa mara tu kinapotokea na taarifa hiyo iambatane na sababu zinazopelekea kifo kutokea pamoja na hatua zilizofanyika kuokoa maisha ya mama na mtoto.” Alisema Mkuu wa mkoa Mtwara.
Katika hatua nyingine, Halmashauri ya Mji Nanyamba imepokea tuzo ya kombe kwa kuibuka kidedea kwa kuvuka lengo la ukasanyaji damu salama kwa asilimia 171.Kikao kazi hiko kimewakutanisha wakurugenzi wa Halmashauri zote saba za wa Mtwara pamoja na wakuu wa wilaya zote (Mtwara, Tandahimba, Newala, Masasi na Nanyumbu); pia kikao kimewakutanisha watumishi wa afya pamoja na waganga wakuu wa hospitali, miji na wilaya za Mtwara.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.