KIKAO CHA TATHIMINI YA UTEKELEZAJI WA VIASHIRIA VYA MKATABA WA AFUA ZA LISHE ROBO YA NNE CHAKETI.
Afisa Tarafa wa Nanyamba kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Abdallah Mwaipaya leo tarehe 25 /7/2025 ameshiriki kikao cha tathimini ya utekelezaji wa viashiria vya mkataba wa afua za lishe ngazi ya kata robo ya nne katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Ndugu Seif Nanyembe amepongeza jitihada zinazofanywa na ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba kwa Kushirikiana na Ofisi ya Mganga Mkuu kitengo cha Lishe chini ya Afisa lishe Pilly Abdul kwa jitihada zinazofahyika katika utekelezaji wa viashiria vya mkataba wa afua za lishe kwa kata zote 17 zilizopo Halmashauri ya Mji Nanyamba.
Aitha ndugu Seif Nanyamba amewapongeza watendaji wa kata kwa jitihada wanazofanya katika kutekeleza viashiria vya Mikataba ya Afua za lishe kwa kuthamini jitihada hizo.
Ofisi ya Mganga Mkuu Kitengo cha Lishe kimewapatia vyeti maalumu Watendaji wote kama ishara ya kuthamini mchango wao katika Shughuli za lishe.
Mbali na hayo Ndugu Seif Nanyembe amenukuliwa akisema kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Ndugu Abdallah Mwaipaya amepokea Mahindi kutoka Chama kikuu cha ushirika (MAMCU) ambayo yatapelekwa shule mbalimbali kwenye kila kata Kama jitihada za kuunga mkono jitihada za afua za lishe.
Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mji Nanyamba Ndugu Walyama Tundosa amewapongeza watendaji hao katika jitihada wanazozifanya waongeze juhudi kufikia lengo la Serikali lililokusudiwa.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.