Mnamo tarehe 23/12/2024, Halmashauri ya Mji Nanyamba imefanya kikao na lengo la kuutambulisha mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari ya Amari. Utambulisho huo ulifanywa kwa kamati ya ujenzi na mapokezi.
Aidha, mwakilishi wa Mkurugenzi katika kikao hicho cha utambulisho wa mradi Mhandisi AMIRI MTUMUSHA ambaye pia ni Mhandisi kutoka Ofisi ya ujenzi Halmashauri ya Mji Nanyamba alisema kuwa mafundi wote wameshakabidhiwa maeneo yao kama walivyoomba na sasa kazi ya ujenzi inatakiwa kuanza mara moja .
Baadhi ya mafundi walioshinda zabuni hiyo ya ujenzi wamehaidi kwa serikali kujenga kwa umakini na viwango vinavyotakiwa na serikali na kuweza kukamilisha kwa wakati unavyotakiwa.
Pamoja na mambo mengine katika kikao hicho wajumbe/ viongozi walihimiza uadilifu, umakini na ufanisi kwa lengo la kuona ujenzi unafanyika kwa wakati, majengo imara na ufanisi mkubwa.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.