Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Ahmed Abbas leo tarehe 25/01/2024 ameongoza zoezi la upandaji miti ikiwa ni maadhimisho ya kampeni ya upandaji miti mkoa wa Mtwara.“Taasisi za elimu, jeshi, viwanda na wengine wenye matumizi makubwa ya mkaa na kuni kama nishati kuanza kutumia nishati mbadala kama gesi ili kupunguza uchafuzi wa mazingira lakini pia uharibifu wa misitu yetu.” Amesema RC Abbas.
Aidha, Mkuu wa mkoa Mtwara amewataka viongozi na wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo kuendelea kuhamasisha uhifadhi wa mazingira kwa kuendelea kupanda miti ili kutekeleza lengo la kila Halmashauri kupanda milioni 1.5 kwa kila mwaka.
Zoezi hilo la upandaji miti kimkoa limefanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ambapo jumla ya miche ya miti 4,445 imepandwa.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka 2024 ni “TUNZA MAZINGIRA, OKOA VYANZO VYA MAJI KWA USTAWI WA VIUMBE HAI NA UCHUMI WA TAIFA”
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.