Jumla ya Watahiniwa 2,566 wavulana 1,126 na wasichana 1,440 sawa na Mikondo122 wanafunzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba wanatarajia kufanya mtihani wa Taifa wa kuhitimu darasa la saba utakaoanza kufanyika tarehe 11 na 12 Septemba 2024 kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA)
Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya Mitihani Halmashauri ya Mji Nanyamba, Mhandisi Mshamu A. Munde, amebainisha kuwa Mtihani huo wa Taifa unajumuisha shule za msingi 64, ikiwa shule zote ni za Serikali hakuna shule ya Mtu Binafsi.
Ameeleza kuwa, tayari maandalizi yote yalifanyika kwa mujibu wa taratibu za Mitihani ya Taifa huku wanafunzi na walimu wameshapewa mafunzo ya usimamizi wa mtihani huo.
Mwenyekiti huyo wa kamati ya Mitihani Mhandisi Munde amewataka wasimamizi wa mitihani kuzingatia Kanuni, Sheria na Taratibu wakati wote wa mitihani na kutokujiingiza kwenye aina yoyote ya vitendo vya udanganyifu kwa kuwa, lengo la mitihani hiyo ni kuwapima wanafunzi kulingana na kile walichojifunza kwa miaka yote saba wakiwa katika shuleni zao.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Divisheni ya Elimu Msingi na Awali Mwalimu Joseph Mhagama amesema kuwa walimu wamewaandaa wanafunzi hao vema kisaikolojia, kiakili na kimwili ili kuwajengea uwezo wa kujiamini wakati wote wa mitihani yao kwa kuwa mtihani huo ni sawa na mitihani mingine waliyokuwa wakifanya mara Kwa mara Waheshimiwa Madiwani, Menejimenti na Watumishi wa Mji Nanyamba unawatakia wanafunzi wote kila la kheri katika mitihani yao
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.