Katika kuadhimisha kilele cha Siku ya Unyonyeshaji maziwa ya Mama Duniani, Halmashauri ya Mji Nanyamba leo tarehe 07 Agosti 2025, imetembelea kata ya Nitekela kijiji cha Maendeleo na Nitekelea Mjini kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa mtoto mchanga na mchanga anayeendelea kukua.
Mgeni rasmi katika tukio hili alikuwa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Nanyamba, Dkt. Dickson Masale, akiambatana na timu ya wataalamu Lishe Halmshauri ya Mji Nanyamba Bi Pilly Abdul na Bi Doris Mselela
Katika hotuba yake, Dkt. Masale alieleza kuwa unyonyeshaji wa maziwa ya mama ni msingi muhimu wa afya ya mtoto, hasa katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo. Alisisitiza kuwa watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya kwanza huwa na kinga imara dhidi ya maradhi, ukuaji mzuri wa mwili na ubongo, na hupata ukaribu wa kihemko na mama wao.
Elimu iliyotolewa Wakati wa maadhimisho haya, wataalamu walitoa elimu juu ya:
Umuhimu wa kumpatia mtoto maziwa ya kwanza ya mama baada ya kuzaliwa
Unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee bila ya kitu chocjote kwa miezi 6 ya mwanzo
Jinsi ya kunyonyesha mtoto na mikao mizuri ya kumuweka wakati wa kunyonya
Madhara ya unyonyeshaiji Mbaya kwa mtoto
faida ya unyonyeshai kwa mtoto na Mama
Kilele hicho kimeambatana na upimaji wa Hali ya lishe kwa watoto na utoaji wa Minyoo ya Tumbo na Matone ya Vitamini A
Wananchi wa kata ya Nitekela walipata fursa ya kuuliza maswali na kushiriki majadiliano yaliyolenga kubadilisha mitazamo na kuimarisha tabia chanya kuhusu unyonyeshaji.
Kaulimbiu ya mwaka 2025:
"Thamini unyonyeshaji: Weka mwzingira wezeshi kwa mama na mtoto''
Maadhimisho haya yameonesha dhamira ya dhati ya Halmashauri katika kuhakikisha kila mtoto anapata haki ya afya bora kuanzia siku ya kwanza ya maisha yake.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.