Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Mhe Abdallah Dadi Chikota katika kuhakikisha huduma ya Afya inapatikana sehemu zote za kutolea huduma ya Afya vizuri Jana tarehe 27/12/2024 amekabidhi gari ya wagonjwa katika kituo Cha Afya Majengo kata ya Njengwa.
Akikabidhi gari ya wagonjwa mbele ya Wananchi alisema kuwa gari hiyo si yake bali gari ya Wananchi inapaswa kutunzwa kwa kila mwananchi ili isaidie kusudio ya huduma hiyo alimalizia kwa kusema maneno hayo.
Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Njengwa Mheshimiwa Moza Kapela alimshukuru Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mbunge kwa kuona umuhimu wa kuleta gari hiyo ili iweze kutumika katika kituo hicho Cha Majengo.
Nae Mganga Mfawidhi w kituo hicho Dkt Jumanne R. Salum ameishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kuwaletea usafiri huo hakusita kueleza kuwa maelekezo yote aliyopewa atayafanyia kazi ikiwa kafanyia matengenezo na kukaa kituo gari hiyo na kutotumia nje ya matumizi husika.
Baadhi ya Wananchi waliokuwa katika hafka hiyo ya makabidhiano ya gari hiyo wamesema kuwa hawana Cha kuwalipa viongozi hao bali watawalipa kwa vitendo muda ukifika
Halmashauri ya Mji Nanyamba ina jumla vituo vya vya Afya vinne vinavyotumika na Hospital moja katika vituo vituo hivyo vya Afya viwili vina magari ya wagonjwa na hospital Mhe Chikota alisisita wataendelea kupambana kila kituo cha afya kuhakikisha kinakuwa na gari yake ya wagonjwa.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.