KONGANI YA VIWANDA KATIKA KIJIJI CHA MARANJE KATA YA MTINIKO KUBANGUA KOROSHO ZAIDI YA TANI 300,000 KWA MWAKA.
Halmashauri ya Mji Nanyamba itanufaika na mradi wa kongani ya viwanda, miundombinu hiyo inayojengwa katika kijiji cha Maranje Kata ya Mtiniko kamati ya siasa Mtwara Vijijini leo tarehe 10/1/2025 imetembelea eneo hilo la Kongani na kuona shughuli zinazoendelea katika eneo hilo.Akisoma taarifa hiyo kwaniaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Mhandisi Sebastian Kiyoyo alisema kuwa hadi mradi huo kukamilika utagharimu kiasi cha bilioni mia mbili tisini na sita milioni mia tano sitini na tano (296,565,000,000), mrsdi unatarajiwa kukamilika kwake kwa muda wa miaka mitatu.
Mhandisi Kiyoyo aliendelea kusema kuwa awamu ya kwanza ujenzi wa maghala mawili ambayo yatabeba ujazo wa tani elfu kumi kila ghala moja, miundombinu ya maji, Umeme pamoja na barabara urefu wa kilomita 11.
Kamati ya hiyo ya Siasa ikiongozwa na Cde Hamisi Wanyama imetoa maelekezo kwa mkandarasi kampuni ya Maragarasi Enterprises Company Limited kuwa mradi huo uwanufaishe wazawa waliojitolea kutoa maeneo hayo kutokana wamelipwa fedha ya kifuta jasho na si fidia kwahiyo kazi za usaidizi wapewe wazawa wa maeneo husika na si kutoka nje ya maeneo hayo.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.