Katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru Tanzania Bara Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba ameongoza zoezi la kufanya usafi na kuchangia Damu kituo cha afya Dinyecha kata ya Dinyecha na Watumishi wa Mji huo wa Nanyamba leo tarehe 8/12/2024.
Kilele cha Maadhimisho hayo ya miaka 63 ya Uhuru yatakuwa tarehe 9 Desemba 2024 kaulimbiu ya mwaka 2024 isemayo "Uongozi Madhubuti na Ushirikiano wa Wananchi ni Msingi wa Maendeleo Yetu".
Mkurugenzi Munde amewataka wananchi wa Mji Nanyamba kuwa na moyo wa uzalendo linapotokea jambo la kujitolea wasiwaachie watumishi peke yao kufanya. Kazi za Kijamii pia aliwahasa wananchi hao kuiunga Serikali ya awamu ya sita kwa juhudi zinazofanywa kwa kuleta fedha nyingi za miradi mbalimbali katika sekta zote iwe maji, kilimo, afya, elimu, barabara na utawala.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.