Ndugu masumbuko mtesigwa afisa mazingira wa halmashauri ya mji nanyamba
Alivyotembelea wavuvi na wafugaji kata ya mnongodi kijiji cha kilimahewa bwawa la tandandia kusikiliza kero za wavuvi na kutolea majibu.
Wavuvi na wafugaji walitoa kero zao kama wakilipa kodi hawapewi risiti, ukosefu wa makazi ya kupumzika pindi wanapotoka kuvua.
Kwa upande wa wafugaji na wakulima kuna mgogoro, kwa wakulima kulalamika kuwa wafugaji wanalisha mazao yao,wakati wafugaji wakitafuta eneo la malisho na maji.
Maelekezo kutoka kwa kaimu mkurugenzi kwa wavuvi ,wafugaji na wakulima.kuhusu wavuvi eneo la kupumzika amewaomba waimarishe ukusanyaji wa mapato na wahakikishe wanapotoa ushuru wapewe risiti na kuanzia tarehe 08/09/2020 zoezi zima la ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa bwawa la ulongwe utafanywa na halmashauri.
Kaimu mkurugenzi alisisitiza utunzaji wa mazingira kama vile uchimbaji wa vyoo, utunzaji wa vyanzo vya maji na ukataji ovyo wa miti, pia alisisitiza kuimarisha ulinzi na usalama katika eneo husika, pia alipinga vikali matumizi ya madawa ya kulevya, matumizi ya pombe kali {gongo}na bangi ili nguvu kazi ya taifa isipotee.
Kaimu mkurugenzi alisisitiza ulinzi na usalama kwa wakazi wote wa eneo ambao wapo karibu na mpaka wa tanzania na msumbiji,kila mwananchi awe mlinzi wa mwenzake na kutoa taarifa kwa viongozi pindi watakapoona mtu yoyote wasio mfahamu na kumtilia mashaka.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.