Siku ya wanawake duniani maarufu kwa jina la ‘’Womens Day’’ imeadhimishwa katika Halmashauri ya Mji Nanyamba, ambapo watumishi na wadau mbalimbali wameshiriki katika kufanya usafi katika kituo cha Afya Dinyecha.
Mgeni rasmi alikuwa makamu mwenyekiti Mhe Diwani Maliki H Majali, ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea wodi la wazazi na kugawa zawadi kwa akina mama mbalimbali waliojifungua katika siku hii.
Aidha akizungumza na wadau mbalimbali wakiwamo watumishi wa Halmashauri, Wanafunzi wa Sekondari ya Nanyamba Day, Viongozi mbalimbali na akina mama waliokuwepo katika eneo hilo, alikemea vikali unyanyasaji wa wanawake katika jamii, maofisini na hata katika maeneo ambayo huduma mbalimbali zinatolewa.
Awali Mhe. Diwani alizungumzia mambo mbalimbali ambayo kwa namna moja au nyingine yamekuwa kikwazo katika kumkomboa mwanamke na kuitaka jamii ibadilike, mfano unyanyasaji wa kijinsia, kutopewa nafasi sawa ya kusoma kwa mototo wa kike na kutokuwepo kwa fursa sawa za kimaendeleo miongoni mwa wanajamii wenyewe, licha ya serikali kupambania usawa.
Mhe Diwani Maliki H Majali akigawa zawadi ya sabuni kwa akinamama waliojifungua siku ya wanawake duniani kitu cha Afya Dinyecha.
Mhe Diwani Maliki H Majali akiwa katika picha ya pamoja na watu mbalimbali waliokuwepo katika maadhimisho ya siku hii ya wanawake duniana.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba Ndugu Geophrey Martini, akimpa zawadi mwanafunzi Rosemary Hassan aliyejibu swali kiufasaa linalohusu maswala ya rushwa, ambalo liliulizwa na Mgeni rasmi Mhe Diwani Maliki H Majali.
Mhe Diwani Maliki H Majali akimpa zawadi ya redha mwanafunzi Rosemary Hassan aliyejibu swali kiufasaa linalohusu maswala ya rushwa siku ya maadhimisho ya wanawake duniani
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.