MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA NANYAMBA WAPATIWA MAFUNZO
Kuelekea zoezi la Uboreshaji wa daftari la Kudumu la mpiga Kura, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya kata leo tarehe 21 /1/2025 wamepatiwa mafunzo katika ukumbi wa Halmashauri wakihimizwa kufanya kazi kwa waledi na uwajibikaji mzuri kuelekea zoezi hilo nzito la kitaifa.Akifungua mafunzo hayo ya siku mbili Afisa Mwandikishaji wa jimbo la Nanyamba Ndg Zefrin Mwenda aliwaeleza kuwa zoezi hilo linahitaji kuwa makini ili liweze kufanyika kwa usahihi unaotakiwa ili watakapoenda kusimamia katika maeneo yao dosari zitakazokuwa zinajitokeza waweze kuzitatua kwa wakati na haraka kwahiyo wameaminiwa na Serikali waoneshe uhaodari wao alimalizia kwa kusema.Zoezi hilo la Uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura ni hatua ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani zoezi hilo linatarajiwa kuanza tarehe 28/1/2025 hadi tarehe 3/2/2025 kauli mbiu isemayo "KUJIANDIKISHA KUWA MPIGA KURA NDIYO MSINGI WA UCHAGUZI BORA".
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.