Katika kuhakikisha maonesho ya siku ya Nanenane mwaka huu yanakuwa ya mfano wa kuigwa kama kauli mbiu ya mwaka huu inayosema "Zalisha kwa tija mazao na bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati "Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba Ndugu, Oscar .A. Ng'itu,(watatu kulia), Wakuu wa Idara mbalimbali na Vitengo, leo wametembelea eneo la jengo la Halmashauri hiyo lililopo Ngongo mkoani Lindi ili kujiridhisha na shughuli mbalimbali za maandalizi ya maonesho ya siku ya Nanenane ambayo Kitaifa mwaka huu yanafanyika Mkoani Lindi kwa mara ya nne mfululizo.
Aidha watendaji hao wakuu wakiwa katika jengo hilo la Halmashauri ya Mji Nanyamba, wamejionea namna Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika pamoja na Idara ya Mifugo na Uvuvi zilivyojipanga vizuri katika Maonesho hayo ambapo Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika Ndugu, Martina Pangani, Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Ndugu, Eliasi Matoja pamoja na Afisa Kilimo Bwana,Michael Kigosi waliwatembeza katika maeneo mbalimbali ya vipando na mabanda ya mifugo vilivyopo katika jengo hilo ikiwa ni pamoja na bustani za mboga mboga, matunda, eneo la ufugaji wanyama na bwawa la kufugia Samaki.
Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba akiongea na wakuu wa Idara na Vitengo, aliagiza Idara zote kuhudhuria na kuandaa maonesho ya shughuli za kila Idara ikiwa ni pamoja na kuwaomba wadau mbalimbali wa maendeleo, vikundi na Taasisi mbalimbali kushiriki maonyesho hayo katika jengo la Halmashauri ya Mji Nanyamba ambayo yataanza rasmi tarehe 1/8/2017 na kufikia kilele tarehe 8/8/2017. Kwa matukio katika picha bofya hapa
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.