MADIWANI wa halmashauri ya mji wa Nanyamba wamepewa mafunzo ya kanuni za kudumu na utawala bora ili waweze kutumia mbinu walizofundishwa kujenga ushwawishi kwa wananchi kushiriki vyema katika mchakato wa maendeleo.
Waheshimiwa madiwani pichani wakifuatilia mafunzo kwa umakini zaidi
Akiongea na Afisa Habari wa Mji, mmmoja ya wawezeshaji wa mafunzo hayo Wakili Prosper Kisinini ambaye pia ni mwanasheria wa Halmashauri ya Mji Nanyamba, amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea viongozi hao mbinu za ushawishi kwa kuwashirikisha wananchi katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. Aidha, kuwajengea ufahamu juu ya kanuni za kudumu ambazo hutumika kuendesha vikao mbalimbali kwa ngazi ya Halmashauri, Kata na Mitaa.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Nanyamba, Mhe. Malik Majali akifunguo mafunzo ya kanuni za kudumu
Afisa habari pia amezungumza na baadhi ya madiwani walioshiriki katika mafunzo hayo ambapo mbali na kuipongeza Halmashauri kwa kuwajengea uwezo katika utendaji kazi katika majukumu yao ya kila siku kutokana na kanuni na miongozo mbalimbali lakini pia yamewawezesha kuwasaidia kutambua mipaka ya kazi kati ya wenyeviti wa Serikali za mitaa na madiwani.
Mafunzo hayo kwa madiwani Nanyamba mji yameandaliwa na halmashauri ya Mji Nanyamba chini ya Idara ya Utumishi na Utawala pamoja na Kitengo cha Sheria..
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.