Mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata Halmashauri ya Mji Nanyamba yahitimishwa rasmi leo, tarehe 6 Agosti 2025, Mafunzo hayo yalifanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa halmshauri yakilenga kuwajengea uwezo wahusika kuhusu majukumu yao wakati wa uchaguzi Mkuu 2025.
Mgeni rasmi katika hotuba ya kufunga mafunzo hayo Msmamizi Msaidizi ndugu Joseph C. Mhagama aliwahimiza wasimamizi hao kuwa waadilifu, waaminifu na wazingatie sheria, kanuni na miongozo ya uchaguzi na kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa vituo, wasimamizi wasaidizi na makarani kwa weledi.
Pia mgeni rasmi aliwasisitiza kusimamia vifaa na rasilimali zote walizopatiwa pamoja na kuhakiki vifaa hivyo kabla na baada ya kutolewa.Aidha, mgeni rasmi aliwapongeza Maafisa wote wa uchaguzi wa jimbo la Nanyamba pamoja na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata kwa utulivu mkubwa toka siku ya kwanza ya mafunzo hayo.
Kwa upande wao, washiriki wa mafunzo hayo walieleza kuwa wamefaidika sana kwa kupata uelewa wa kina kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi, na wako tayari kutekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa.
Uchaguzi Mkuu 2025 kauli Mbiu isemayo ''Kura yako ni haki yako jitokeze kupiga kura''
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.