Leo tarehe 04 Agosti 2025, mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata yamefunguliwa rasmi katika ukumbi wa halmashauri Mji Nanyamba.
Mafunzo haya ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu 2025, yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo wasimamizi wasaidizi katika kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu, na kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Ndg Hashimu Kazoka ambaye Msimamizi Wa Uchaguzi Jimbo la Nanyamba katika hotuba yake alisisitiza umuhimu wa watendaji hao kuzingatia misingi ya haki, usawa na uwazi katika utekelezaji wa majukumu yao.
"Mnafanya kazi muhimu sana kwa taifa letu. Uchaguzi ni moyo wa demokrasia, hivyo mafunzo haya yawatayarishe kisaikolojia na kitaalamu ili kutekeleza kazi zenu kwa ufanisi na bila upendeleo," alisema Mgeni Rasmi.
Aidha, alitoa wito kwa washiriki wote wa mafunzo hayo kuhakikisha wanazingatia maadili ya kazi, kuepuka upendeleo wa aina yoyote na kutunza siri za uchaguzi kwa mujibu wa sheria.
Mafunzo hayo yatafanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo tarehe 4-6 Agosti 2025 yakijumuisha mada mbalimbali za sheria za uchaguzi za mwaka 2025
Mafunzo haya yanajumuisha wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kutoka kata zote 17 ndani ya halmashauri na yanatarajiwa kuleta ufanisi mkubwa katika uendeshaji wa uchaguzi huo.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.