Mapema leo tarehe 11/2/2025 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba Daktari Dickson Masale amefungua mafunzo maalum kwa walimu wa Afya katika shule zote za Msingi zilizopo Halmashauri ya Mji Nanyamba kuhusiana na magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele katika jamii.Akizungumza Mratibu wa Magonjwa Ambayo hayapewi kipaumbele Ndugu Vitalisi Lai amesema kuna aina mbalimbali za Magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele katika jamii ikiwa ni usubi, matende, mabusha, kichocho, minyoo ya tumbo na trakoma.
Aidha mafunzo hayo yaliambatana na ugawaji wa Dawa Maalumu za minyoo na kichocho kwa shule zote za Msingi zilizopo Halmashauri ya Mji Nanyamba ambapo siku ya tarehe 12/2/2025 itakuwa ni siku maalumu kwa wanafunzi wote wa Halmashauri ya Mji Nanyamba kupatiwa dawa hizo.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.