Afisa Mwandikishaji wa jimbo la Nanyamba Ndg Zefrin A. Mwenda jioni ya leo amefunga mafunzo hayo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la Mpiga kura ngazi ya jimbo huku akitoa wito kwa maafisa wote waliopatiwa mafunzo kuendelea kutumia muda wao wa ziada kusoma na kupitia maelekezo yote waliyopewa kipindi cha mafunzo hayo.
Aidha aliendelea kuwasihi maafisa hao utunzaji wa vifaa hivyo muhimu kwa niaba ya maaendeleo ya Taifa kwa ujumla na wasitumie utashi kwa jambo lisilo hitaji kutumia utashi wanapokwama waulize kwa wataalam wa vifaa hivyo kwa kufuata miongozo ya Tume huru inavyosema.Mafunzo hayo ya siku mbili yametamatika rasmi leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.