Maafisa kutoka Bank Kuu ya Tanzania tawi la Mtwara leo tarehe 10/12/2025 wametoa elimu kwa watumishi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba ya uwekezaji katika dhamana ya serikali, ambapo wamesema kuna aina mbili ya dhamana za serikali yaani Dhamana za muda mfupi na Dahamana za muda mrefu(Hati fungani). Akitoa mafunzo hayo kwa watumishi wa Mji Nanyamba Afisa toka Bank Kuu ya Tanzania tawi la Mtwara ndugu Simon Kessy amesema kuwa dhamana za muda mfupi huiva ndani ya mwaka mmoja, Kwa kawaida huuzwa kwa bei chini ya shilingi 100 (Discount) na wakati wa kuiva mwekezaji hulipwa shilingi 100. Kiwango cha chini cha kuwekeza katika dhamana hizi ni shilingi 500,000 (Shilingi Laki Tano za Tanzania) na Dhamana za muda mfupi zinazotolewa na Benki Kuu ya Tanzania zinaiva katika vipindi vinne: siku 35, siku 91, siku 182 na siku 364.Dhamana za muda mrefu (Hati fungani) hutolewa kwa ajili ya kugharamia hasa miradi ya maendeleo.
Hati fungani za Serikali za muda mrefu zinazotolewa na Benki Kuu ya Tanzania kwa niaba ya serikali kwa sasa, zinaiva katika vipindi saba: miaka 2, miaka 5, miaka 7, miaka 10, miaka 15, miaka 20, na miaka 25. Zinatolewa katika kiwango cha riba isiyobadilika
Dhamana za Serikali za Muda Mfupi na za muda mrefu zina faida zifuatazo kwa mwekezaji:
• Ni salama kwani Serikali haitarajii kukiuka matengenezo ya wadai wake wakati wa malipo.
• Zinahamishika, hivyo mwekezaji anaweza kuziuza kabla ya muda wake wa kuiva kama anataka kufanya hivyo.
• Dhamana za Serikali zinaweza kutumika kama dhamana kwa ajili ya mikopo.
• Dhamana za Serikali zina kiwango cha faida inayoridhisha.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.