RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amewahakikishia na kuwatoa hofu wakulima wa zao la korosho nchini kuwa, watalipwa fedha zao bila wasi wasi wowote.
Hayo yamesemwa leo na Rais huyo wakati wa uzinduzi na uwekaji na jiwe la msingi katika uwanja wa ndege wa Mtwara uzinduzi ambao umefayika katika viwanja hivyo.
Wakulima waliohakikishwia kulipwa ni pamoja na wale waliokuwa wakidaiwa kununua korosho kinyume na sheria maarufu kama wafanyabiashara wa ‘Kangomba.’
Aidha ahadi hiyo imewagusa pia wakulima ambao korosho zao ni zaidi ya kilo 1500 na kuendelea ambao kwa idadi yao wanakadiriwa kuwa 18 elfu wakati huo huo waliokuwa wananua kinyume na taratibu ni zaidi ya 700.
Hata hivyo serikali imetoa onyo kwa wanunuzi hao wa kangomba kuacha vitendo hivyo na kwamba msimu mwingine haitofumbia macho vitendo hivyo.
Rais huyo alisema kuwa, katika msimu huo serikali iliamua kununua korosho hizo baada ya kuona wanunuzi wanataka kununua kwa bei ya chini kitendo ambacho kinawanyima wakulima.
“Kunuuna korosho kwa bei ya chini ni kuwanyonya wanyohge kwahiyo serikali ikaona ipo haja ya kununua korosho hizo ili kuwasaidia wakulima kupata haki zao vizuri”,Alisema DK. Magufuli
Hata hivyo ametoa agizo kwa viongozi katika mikoa yote inayolima zao hilo kuhakikisha wanasimamia zao hilo ili kumsaidia wakulima ili wapate stahiki zao.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.