Shule ya Sekondari Dinyecha iliyopo kata ya Dinyecha leo tarehe 12/4/2025 wamefanya Mahafali ya 2 toka ianzishwe elimu ya Kidato cha tano na sita, ambapo katika Mahafali hayo yameongozwa na Mgeni Rasmi Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Mhe @chikota_abdallahAkisoma Taarifa ya shule hiyo Mkuu wa shule ya Dinyecha Mwl Mwajuma Mnayahe aliishukuru Serikali kwa kuleta Miundombinu bora yenye thamani ya bilioni 1.2 kwaajili ya kidato cha tano na sita, pia Mwl Mnayahe hakusita kutoa changamoto ya upungufu wa walimu na Ujenzi wa Uzio wa shule kutokana na shule hiyo kuwa ya wasichana tuu wa kidato cha tano na sita.Nae Mis Hapiphania Severine kwaniaba ya wanafunzi wanaohitimu mwaka 2025 pindi anasoma risala hiyo wameishukuru Serikali kwa kujenga shule mbalimbali za kidato cha tano na sita nchi nzima bila kuangalia sehemu maalum, aliaongeza kwa kwa kusema Serikali ya awamu sita wanamuomba Rais Mhe Dkt @samia_suluhu_hassan kuwapatia Gari la kuwawezesha kulitumia katika Shughuli mbalimbali kama vile kupeleka wagonjwa na safari za Kimasomo kwenye mitihani ya ujirani mwema.Aidha Mgeni Rasmi ambae ni Mbunge wa Jimbo la Nanyamba katika Hotuba yake amewapongeza walimu na watumishi wa shule hiyo kwa kufaulisha kwa daraja la kwanza na tatu na kuwaasa wanafunzi hao zaidi ya wanafunzi 200 waotarajia kufanya mtihani mwezi Mei kufuata nyenzo za wenzao waliopita kwa kufaulu vizuri.Mhe Chikota alisema kusema kuwa changamoto zote "mlizotoa nazitambua nitazidi kuzifuatilia kwa ukaribu ili wanafunzi na watumishi wa shule hii mfanye kazi zenu bila kikwazo" alimalizia kwa kusema maneno hayo.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.