Makamu mwenyekiti wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Bi. Zainabu Shomari, leo Tarehe 19.07.2023 ametembelea na kujionea mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari Dinyecha, wenye Thamani Tsh. Bilioni 1.2 unaoendelea katika Halmashauri ya Mji Nanyamba.
Aidha, ameipongeza Serikali ya Dr. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mpana na kusema kuwa ujenzi wa shule hiyo utasaidia kuongeza chachu kwa wanafunzi kutokana na uboreshaji wa mazingira na majengo na kuwaondolea wanafunzi mazingira magumu ya kupata elimu.
Ziara hiyo ameambatana na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi CCM akiwemo Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Mhe. Abdallah Dadi Chikota.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.