Halmashauri ya Mji Nanyamba imepokea fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 1.32 kupitia Programu ya BOOST kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya shule za Awali na Msingi.
Kupitia mapokezi ya fedha hizo Halmashauri inalenga kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa, matundu ya vyoo na ukarabati wa vyumba vya Madarasa ili kuongeza ufaulu na kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba Bi Zainab S. Mgomi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha katika Halmashauri ya Mji Nanyamba.
"Mhe Rais ametupa fursa muhimu kuwezesha miundombinu ya shule zetu inaendelea kuwa bora kwa watoto wetu kusudio waweze kusoma katika mazingira bora tunatoa ahadi kwake kusimamia fedha hizi kwa weledi na kukamilisha miradi kwa wakati kama ilivyokusudiwa alimalizia kwa kusema maneno Bi Zainab Mgomi"
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.