Afisa kilimo kaika Halmashauri ya Mji Nanyamba Bw, Chelesi akielezea mbinu bora za upandaji wa Mahindi Katika nafasi inayokubalika kitalaamu kwenye maonesho ya Nanenane Ngongo Mkoani Lindi tarehe 3/8/2017
Katika Kuhakikisha wananchi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba wanakuwa na ziadaya ya chakula cha kutosha kwa mwaka mzima wameshauriwa kufuata mbinu bora za kilimo.
Hayo yameelezwa na Afisa kilimo kutoka Halmashauri ya Mji Nanyamba Bw, Chelesi kwenye maonesho ya Nanenane Ngongo Mkoani Lindi tare 3/8/2017.
Awali Afisa huyo akitoa maelezo kwa wageni mbalimbali waliotembelea jengo na Bustani za Mfano za Halmashauri hiyo, aliwataka wananchi kufuata taratibu na kanuni bora za kilimo cha zao la mahindi ili kujipatia mavuno ya kutosha kwa ajili ya chakula chao na bishara.
Vilevile alihimiza wananchi kutumia taratibu na kanuni bora za kilimo cha zao hilo ikiwa ni pamoja na kutumia aina bora za mbegu wanazoshauriwa na wataalamu, kupanda kwa kutumia vipimo sahihi,\ na kutmia mbolea ili kupata mavuno mengi kwa msimu husika.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.